19 Agosti 2020 - 13:05
Ikhwanul Muslimin yalaani mapatano ya Imarati ya Israel, yasema ni usaliti dhidi ya al Aqsa

Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imelaani hatua ya Imarati ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taarifa iliyotolewa na harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imesema kuwa, kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel ni kusaliti malengo ya Palestina, Msikiti wa al Aqsa na kukanyaga haki za taifa la Palestina.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, juhudi za aina yoyote za kutaka kuziburuta nchi nyingine za Kiarabu katika kinamasi kibaya cha kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel zinapaswa kulaaniwa na kupigwa vita. 

Taarifa ya harakati hiyo kubwa zaidi ya kisiasa ya upinzani nchini Misri imeyataka mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kupinga hatua yoyote ya kuanzisha uhusiano na utawala unaoua raia wasio na hatia wa Palestina.

Ikhwanul Muslimin imesema kuwa, matokeo ya kuanzisha uhusiano na Israel ni uharibifu, kushindwa na kuwa tegemezi. 

Alhamisi iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza habari ya kufikiwa mapatano baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu na utawala haramu wa Israel kuhusu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya pande mbili. Hatua hiyo imelaaniwa na harakati zote za mapambano ya ukombozi wa Palestina na mataifa ya Kiislamu.  

342/